YANGA MATUMAINI KIBAO KUPINDUA MEZA NIGERIA

YANGA MATUMAINI KIBAO KUPINDUA MEZA NIGERIA


 UONGOZI wa Yanga umeweka wazi kuwa upo tayari kwa ajili ya mchezo wa kesho dhidi ya Rivers United ambao ni wa Ligi ya Mabingwa Afrika.

Ni Mchezo wa marudio baada ya ule wa awali uliochezwa Uwanja wa Mkapa ubao kusoma Yanga 0-1 Rivers United.

Ofisa Habari wa Yanga, Haji Manara amesema kuwa wamekwenda nchini Nigeria kufanya kazi na sio kuuza sura huku wakiwa wamejiandaa kwa ajili ya fitina ambazo hufanywa kwenye mechi za kimataifa.

“Hatuendi kuuza sura tunakwenda kufanya kazi hivyo kikubwa mashabiki wa Tanzania dua yao ni muhimu kwani hautakuwa mchezo wepesi.

“Jambo ambalo tunaamini ni kwamba tutarudi kwa ushindi huku tukiwa na furaha ya kuweza kupindua meza kibabe.

“Ni vita ya dakika 90 ndani ya uwanja, vijana wanajua na wanakazi kubwa ya kufanya juhudi na bidii kwa ajili ya kupata matokeo chanya.” amesema.

Msafara wao uliofika salama leo nchini Nigeria ulikuwa na nyota wake wote ikiwa ni pamoja na Yacouba Songne, Heritier Makambo, Dickson Job, Zawad Mauya na Ramadhan Kabwili.

Author:

Leave a Reply

Your email address will not be published.