Saratani ya matezi ni ugonjwa wa aina gani na utaigunduaje?

Saratani ya matezi ni ugonjwa wa aina gani na utaigunduaje?

Dakika 4 zilizopita

Chanzo cha picha, Getty Images

Karibu watu milioni 10 walipoteza maisha mwaka 2020 kutokana na ugonjwa huu, kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Afya Ulimwenguni.

Aina ya saratani ambayo ilisababisha vifo vingi zaidi mwaka jana ilikuwa ya mapafu kwa watu milioni 1.8, lakini iliyosajiliwa idadi kubwa ni saratani ya matiti, ikiathiri kaya milioni 2.26.

Lakini kuna saratani ya damu ambayo inaongezeka na ni kawaida kwa watu wazima: lymphoma.

Septemba 15, Siku ya kutoa uelewa kuhusu saratani ya matezi Duniani, tuliwasiliana na wataalamu ili kujua saratani hii ni nini na jinsi ya kuigundua

Saratani ya matezi ni nini? (Lymphoma)

Kuna makundi matatu makuu ya saratani ya damu: leukemia, myeloma, na lymphoma.

Matezi nayo yako kwenye makundi mawili Hodgkin’s lymphoma na non-Hodgkin’s lymphoma.

Inaitwa hivyo kwa sababu mnamo 1832 iligunduliwa na daktari wa magonjwa wa Uingereza Thomas Hodgkin (1798-1866) baada ya kuchambua watu kadhaa walio na dalili za saratani zilizoathiri tezi za limfu.

Chanzo cha picha, GUY’S HOSPITAL REPORTS

Saratani ya matezi aina ya Hodgkin na isiyo ya Hodgkin

Hapo awali iliitwa “ugonjwa wa Hodgkin” lakini mwishoni mwa karne ya 20 iliitwa jina “Hodgkin’s lymphoma.”

Kama ilivyoelezewa na Chama cha saratani ya damu na matezi ya Marekani, hii ilitokea kwa sababu utafiti uliobainisha kwamba ugonjwa huo ni matokeo ya kidonda kwenye DNA ya lymphocyte ambayo ni aina ya seli nyeupe ya damu, inayohusika na kujilinda dhidi ya maambukizi.

Mabadiliko katika lymphocyte yanaibadilisha kuwa seli ya lymphoma. Hizi huungana na kuunda chembe nyingi za seli, ambazo ni vivimbe na mara nyingi huungana pamoja kwenye tezi la limfu au sehemu nyingine za mwili.

“Tutafikiria kuwa mwili ni kama nyumba na saratani ya damu inaathiri nyumba nzima, wakati saratani ya matezi inaathiri chumba. Katika sehemu moja, sehemu ya mwili, ambayo ni tezi,” daktari anaambia BBC Mundo. Carla Casulo, mkurugenzi wa Programu ya Huduma ya saratani ya matezi katika Taasisi ya Saratani ya Wilmot katika Chuo Kikuu cha Rochester huko New York.

Matezi ya saratani (Hodgkin na non-Hodgkin lymphoma)

Saratani ya matezi aina ya Hodgkin huenea kwa utaratibu kutoka kwa kundi moja la tezi za limfu kwenda kwa nyingine, wakati non-Hodgkin ni aina ya saratani ambayo huenea kupitia mfumo wa limfu kwa njia isiyo ya kawaida, vinaelezea Vituo vya Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa (CDC).

Chanzo cha picha, Getty Images

Namna ya kuigundua saratani ya matezi

Dalili ni pamoja na uvimbe wa tezi za limfu, haswa katika sehemu ya mwili ambapo saratani ya matezi huanza kukua.

Maeneo ya kawaida ambayo tezi za limfu zinaweza kuhisiwa na vidole ni sehemu za siri, kwapa, shingo, nyuma ya masikio, na nyuma ya kichwa. Lakini pia kuna sehemu za tezi za limfu katika sehemu nyingine za mwili kama vile kifua na tumbo.

Chanzo cha picha, Getty Images

Mbali na tezi zilizovimba, dalili za saratani hii zinaweza kuwa sawa na zile za magonjwa mengine, kama vile homa na hata Covid-19.

Hizi ni pamoja na homa, jasho la usiku, uchovu, kukohoa, kuwasha, na kupunguza uzito.

Je! Inaweza kutibiwa na kuponywa?

Saratani ya matezi aina ya Hodgkin ni moja wapo ya aina ya saratani inayoweza kutibiwa. Hadi sasa sababu haijulikani.

Pia haiwezekani kuizuia na huwezi kuipata kutoka kwa mtu mwingine. Kawaida hugunduliwa kati ya umri wa miaka 20 hadi 40 na pia baada ya miaka 60.

Chanzo cha picha, Getty Images

Wakati huo huo, saratani ya matezi isiyo ya Hodgkin, iliyo na aina nyingi, matibabu inategemea sifa zake

“Kwa bahati nzuri, karibu saratani zote za matezi zina tiba. Kuna wachache sana ambao hawawezi kutibiwa (…) lakini kwa bahati mbaya haiwezi kuzuiwa ni ugonjwa mgumu kidogo”, anafafanua daktari Carla Casulo.

Kwa hivyo, wakati unashuku kuwa kuna kitu kibaya mwilini, pendekezo la kawaida ni kumuona daktari.

Source link

Author:

Leave a Reply

Your email address will not be published.