Aucho hatihati kuikosa Mbeya Kwanza

Aucho hatihati kuikosa Mbeya Kwanza
Aucho hatihati kuikosa Mbeya Kwanza

By Saddam Sadick

Mbeya. Licha ya kuwa kikosini na kuendelea na mazoezi na timu kiungo wa Yanga, Khalid Aucho huenda akawa miongoni mwa nyot watakaokosa mchezo dhidi yaMbeya Kwanza katika Ligi Kuu ya NBC.

Timu hizo zinatarajia kukutana kesho Jumanne katika mechi itakayopigwa uwanja wa Sokoine jijini Mbeya saa 10:00 jioni ukiwa wa kwanza kukutana wapinzani hao.

Akizungumza leo Novemba 29, Kocha Mkuu wa timu hiyo, Nasreddine Nabi, amesema Aucho bado haijaeleweka rasmi kama atakuwa kikosini kwa wachezaji watakaocheza mechi hiyo kutokana na kutopona vizuri majeraha lakini hali ya uwanja pia.

Amesema kuwa wachezaji wengine ambao watakosekana kesho uwanjani ni Yanick Bangala mwenye kadi za njano na Yacouba Sogne aliyeumia goti na Jesus Moloko aliyeumia sehemu ya ubavu wakati wa mazoezi.

“Yanga ni kubwa kwahiyo kukosekana kwa mchezaji mmoja kunawapa wengine nafasi kuonesha uwezo wao, kimsingi tumejipanga kushinda mechi hiyo na tunajua ushindani utakuwepo” amesema Nabi.

Nabi PIC

Kocha wa Yanga, Nasreddine Nabi sambamba na Saido Ntibazonkiza wakizungumza na Waandishi wa Habari kuelekea mchezo wa kesho dhidi ya Mbeya Kwanza.

Advertisement

Kocha huyo ameongeza kuwa mipango yao msimu huu ilikuwa ni kushinda mechi zote, lakini mchezo uliopita dhidi ya Namungo walishindwa kufikia malengo kwa kuambulia sare huku akidai kuwa hawajakata tamaa.

Ameongeza kuwa maandalizi ya mechi ya kesho ni tofauti na mchezo uliopita kwani Namungo ni tofauti na Mbeya Kwanza sambamba na hali ya uwanja ni tofauti.

Naye mshambuliaji wa timu hiyo, Said Ntibazonkiza amesema kwa sasa matokeo yaliyopita hawayapi nafasi ispokuwa wanafikiria zaidi mechi ya kesho na kwamba matarajio yao ni kuondoka na pointi tatu.

“Siyo kila siku tutashinda, lakini tulishaelekeza nguvu katika ushindi ndio maana kila mchezo tunapambana kama fainali kutafuta alama tatu, tumejipanga kesho kupata ushindi” amesema Ntibazonkiza.

Leave a Reply

Your email address will not be published.