Kosgei, Chepng’eno wajitosa Nakuru City Marathon 2021

Kosgei, Chepng’eno wajitosa Nakuru City Marathon 2021
Kosgei, Chepng’eno wajitosa Nakuru City Marathon 2021
Kosgei, Chepng’eno wajitosa Nakuru City Marathon 2021

BINGWA wa Dunia wa Marathoni, Brigid Kosgei, ni mmoja wa magwiji wa riadha waliojitosa kwenye makala ya mwaka huu ya mbio za Stanbic Nakuru City Marathon, itakayofanyika kesho, Novemba 28, katika kaunti ya Nakuru.

Kwa mujibu wa Martin Keino, ambaye ni mmoja wa waandaaji wa mashindano hayo, Kosgei anayejivunia muda bora wa dakika 29:54, aliyoisajili kwenye mbio za kilomita 10, katika mashindano ya 2018 Madrid San Silvestre Vallecana, atashiriki mbio za Kilomita 10.

Kosgei anaingia kwenye mashindano haya, akiwa ni mshikilizi wa medali ya fedha ya Olimpiki (2020 Olympics), lakini akiwa ametoka kushiriki London Marathon alipomaliza nafasi ya nne (Oktoba 8). Huko Tokyo, alimaliza sekunde 16, nyuma ya Peres Jepchirchir (2:27:20).

Wakati huo huo, Mwanariadha Viola Chepng’eno, (23), ambaye ni gwiji wa mbio za mita 800, 1000, 1500, 3000, kilomita 10 na 15, pamoja na mbio za nusu marathoni (Km21), amatumaini makubwa ya kufanya poa kwenye mbio za kesho.

Kwa mara ya mwisho, Chepng’eno ambaye amekuwa akijifua huko Keringet (Nakuru) na Olkalou (Nyandarua), kujiandaa na mbio hizi, alishiriki mbio za Eldama Ravine Half Marathon na alimaliza nafasi ya tano, akitumia muda wa saa 1:14.42. “Niko tayari kuweka historia kwenye mbio za Nakuru City Marathon. Nilianzia Keringet kabla ya kuhamia Olkalau na kwa kuangalia maandalizi yangu, naamini niko fiti. Namuomba Mungu kila kitu kiende sawa,” alisema.

Takribani wanariadha 500, wakiwemo wanariadha kutoka Seycheles ambao wanafanyia mazoezi yao huko Iten, wameshajitokeza kushiriki mbio hizi, zinazoandaliwa na Kaunti ya Nakuru, kwa kushirikiana na benki ya Stanbic.

Advertisement

Nakuru City Marathon, itahusisha pia, mbio za familia za kilomita 10 na 5. Washindi wa wanaume na wanawake, Kilomita 21, watajishindia Ksh500,000 huku washindi wa mbio za Kilomita 10, wakiondoka na Ksh100,000.

Leave a Reply

Your email address will not be published.