MATANO: Hatuchomi picha CAF

MATANO: Hatuchomi picha CAF
MATANO: Hatuchomi picha CAF

By Sinda Matiko

KOCHA Robert Matano kaapa yeye ya Tusker yake hawatachoma picha tena hapo kesho watakapochuana na CS Sfaxien kwenye dimba la CAF Confederation Cup.

Tusker FC walichujwa kwa machungu kwenye dimba la CAF Champions League licha ya kuanza vizuri.

Walifuzu kwenye raundi ya kwanza ya mtoano kwa kishindo kwa kuwalima Arta Solar 7 wa Djobouti jumla ya mabao 4-1.

Hii ni kabla ya kudhalilishwa na Wamisri Zamalek kwenye raundi ya pili ya mtoano kwa kulimwa jumla ya magoli 5-0. Hatua hiyo iliwasukuma hadi kwenye CAF Confederation.

Na sasa kesho wakiwa wanakutana na Watunisia Sfaxein ambao ni mabingwa mara tatu wa CAF Confederation 2007,2008 na 2013, Matano anadai, hatakubali kufedheheshwa tena ukizingatia kuwa wanacheza nyumbani.

“Kila aliye kambini anategemea matokeo mazuri Jumapili. Tumekuwa tukifanya mazoezi makali kwa wiki mbili zilizopita. Katika kipindi hicho pia tumeshiriki mechi kadhaa za kirafiki zilizotuwezesha kujigeji. Tunajua mapungufu yetu yako wapi kwa sasa.” Matano kachocha. Kocha huyo mzoefu anasisitiza kuwa kesho itakuwa ni mechi ya kufa mtu na wala ubabe wa Watunisia hao hauwatishi.

Advertisement

“Hawatutishi, kesho tuna kazi moja tu, kufunga magoli ya kutosha. Hatuwezi kuwa tunacheza nyumbani kisha tushindwe kusajili matokeo ya heshima. Sio safari hii.” kaongeza. Kuelekea mchuano wa kesho, Matano ana kikosi chake kizima isipokuwa tu fulubeki Jimmy Mbugua anayeuguza jeraha la enka.

Leave a Reply

Your email address will not be published.