Mwamuzi wa mechi ya Namungo na Yanga afikishwa kwa pilato

Mwamuzi wa kati wa mchezo wa Namungo FC dhidi ya Yanga SC, Abel William kutoka Arusha amepelekwa kwenye Kamati ya Waamuzi ili shauri lake likajadiliwe na kamati hiyo.

Uamuzi huo umekuja baada ya Kamati ya Uendeshaji  na Usimamizi wa Ligi Kuu kujiridhisha kuwa mchezo husika ulikumbwa na  na matukio na maamuzi yalioacha  maswali juu ya ya utekelezaji wa sheria 17 za mpira  wa miguu.

Kamati imetoa onyo kali kwa wachezaji wa Namungo FC, Jacob Massawe, Lucas Kikoti na Bigirimana Braise ambao kwa nyakati tofauti walionyesha utovu wa nidhamu kwa vitendo na lugha.

Katika hatua nyingine, Kamati imewapongeza wachezaji wa klabu ya Namungo Obrey Chirwa na Abdulmalik Adam Zakaria  kwa kuonesha vitendo vya uungwana  mchezo ambapo  walionekana wakiwazuia  wachezaji wenzao  wasimzonge na kumtolea lugha chafu  mwamuzi.

The post Mwamuzi wa mechi ya Namungo na Yanga afikishwa kwa pilato appeared first on Bongo5.com.

Author:

Leave a Reply

Your email address will not be published.