Mwangemi ni kutua Camp Nou ama Etihad

Mwangemi ni kutua Camp Nou ama Etihad
Mwangemi ni kutua Camp Nou ama Etihad

By Abdulrahman Sheriff

MOMBASA. BEKI wa Bandari FC, Boniface Mwangemi ana nia kubwa ya kuhakikisha anatua uwanja wa Camp Nou ama Etihad.

Mwangemi amesema jana kuwa anafanhya bidii kuinua kipaji cha uchezaji wake kwa makusudi ya kutaka kuichezea Barcelona ama Manchester City lakini kama hakubahatika kupata fursa ya kuzichezdea timu hizo mbili, atapendelea kuchezea timu yoyote huko Bara Ulaya.

Akiongea na Mwanaspoti, Mwangemi anayetarajia kufika umri wa miaka 19 hapo Desemba 19 amesema amefurahikia mno kusajiliwa na Bandari FC naana imani kocha Andre Cassa Mbungo ataweza kumtengeneza na kuwa na kipaji cha kucheza soka la kulipwa huko ng’ambo.

“Nafurahikia mno na jinsi tunavyopewa mafunzo na kocha wetu kwani nimeingiwa na imani kubwa kuwa katika kipindi kijacho, nitakuwa mchezaji wa kuaminika na hata kuchaguliwa katika kikosi cha timu ya taifa ya Harambee Stars,” akasema Mwangemi na kuongeza;

“Ninaamini jinsi tunavyofunzwa na mkufunzi wet una tukitia bidii za kibinafsi, wengi wetyu tutafika mbali. Nia yangu kubwa nataka kuichezea timu ya Barcelona ama Manchester City ama kama si hizo, nichezee timu yoyote ya Bara Ulaya,” akasema.

Amesema kitu kilichomfurahisha zaidi kuwa na Bandari ni kuwa wachezaji wenzake na maofisa wanampokea vkizuri mchezaji na kumfanya asijione kuwa mgeni. “Kwa kipindi kifupi, nimejiona kama niliyekuja miaka kadhaa katika kikosi hiki cha Bandari,” akasema.

Advertisement

Mwangemi anasema kama walivyo na nia wachezaji wenzake wote wa Bandari, pia naye ana ham una atafanya bidii kuisaidia timu yake hiyo kupata ushindi na kuwa mabingwa wa Ligi Kuu msimu huu.

“Naamiani tunaweza kutwa taji la ubingwa kwani timu yetu ni nzuri,” akasema.

Leave a Reply

Your email address will not be published.