Mzozo wa Tigray: Tuhuma na kujitolea huku mapigano ya Ethiopia yakienea

Mzozo wa Tigray: Tuhuma na kujitolea huku mapigano ya Ethiopia yakienea

Dakika 7 zilizopita

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha,

Volunteers conduct a night patrol on the lookout for suspicious activity earlier this month

Baada ya giza kuingia, katika kitongoji cha makazi katika mji mkuu wa Ethiopia, Addis Ababa, makumi ya raia wa kujitolea walikuwa na shughuli nyingi wakizunguka mitaa yao usiku mmoja wiki iliyopita, wakisimamisha na kupekua magari na kuangalia hati.

“Kamati yetu ya kitongoji inajumuisha watu wapatao 180. Tumewakamata watu wengi. Na tumegundua vitu vingi vya kutia shaka, zikiwemo bunduki na vilipuzi,” alisema mzee mmoja aliyeonekana kuratibu upekuzi huo.

Wafanyakazi wa kujitolea wanawasaka waasi wa Tigray, na wafuasi wao, chini ya kanuni mpya za hali ya hatari zilizoanzishwa na serikali ya Ethiopia ili kukabiliana na mashambulizi ya kijeshi ya Tigray.

Wakosoaji wanasema maelfu ya watu wamezuiliwa isivyo haki, lakini ukandamizaji huo unaonekana kuungwa mkono na watu wengi katika mji mkuu.

“Fanya haraka, anajaribu kutoroka,” mtu mwingine alisema, ghafla, akiongea kwenye simu yake ya mkononi.

Barabara chache kutoka hapo, kikundi kipya cha wafanyakazi wa kujitolea walio wazee walikuwa wamekusanyika kwa ajili ya mafunzo, wakitembea kwa hatua zaidi au kidogo na kusikiliza maagizo.

Hali kwa ujumla katika mji mkuu inaonekana kuwa shwari. Ingawa Uingereza na nchi nyingine zimeonya kwamba hali ya usalama “inazorota,” kama wapiganaji wa Tigray na makundi mengine ya waasi yanaripoti kwamba wanasonga mbele kuelekea Addis, ubalozi wa Urusi ulituma ujumbe tofauti sana kwenye mitandao ya kijamii.

Ilitangaza kwamba “kuanzishwa kwa hali ya hatari hakujaleta mabadiliko yoyote muhimu kwa maisha ya kila siku ya mji mkuu wa Ethiopia.”

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha,

Waziri mkuu ana cheo cha luteni kanali katika jeshi

Waziri Mkuu wa Ethiopia, Abiy Ahmed, hivi karibuni alitangaza kuwa anaelekea kwenye mstari wa mbele kuongoza wanajeshi wake.

Picha za video, zilizotolewa na serikali, zilimuonesha akiwa amevalia sare akiwa amezungukwa na wanajeshi, inaonekana katika eneo kame la Afar kaskazini mashariki mwa mji mkuu.

“Sasa tumefaulu kusafisha eneo hilo kabisa,” Waziri Mkuu Abiy alisema kwenye picha hiyo.

“Hamasa ya vikosi vya ulinzi ni kubwa sana. Tutaendelea hadi uhuru wa Ethiopia uhakikishwe,” aliendelea.

Waziri Mkuu alisema wanajeshi wake wako mbioni kuteka miji kadhaa kutoka kwa kundi la Tigray People’s Liberation Front (JWTZ).

Lakini madai hayo ni magumu kuthibitisha kwa upatikanaji na mawasiliano katika maeneo ya migogoro yaliyowekewa vikwazo, na kuanzishwa kwa sheria mpya zinazozuia uchapishaji wa harakati zozote za kijeshi au “matokeo ya uwanja wa vita” ambayo hayajaidhinishwa na serikali.

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha,

Mwanamume aliyebeba bendera ya Tigray akisherehekea mafanikio ya eneo la JWTZ mwezi Juni

Maafisa wa TPLF – ambao hivi majuzi walichapisha picha za maelfu ya wafungwa wa kivita wa Ethiopia – wanasisitiza kuwa wanaendelea kusonga mbele katika nyanja kadhaa, huku wakilenga zaidi mji mkuu wa Debre Birhan, unaoonekana na wengi kama eneo kuu la mwisho la ulinzi la Ethiopia nje ya mji mkuu.

Watu wanakuwa katika hali ‘mbaya’

Bila kujali ni upande gani unashinda, ni wazi kwamba mzozo unaenea, na pamoja na hayo, mgogoro wa kibinadamu wa Ethiopia.

Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) sasa linakadiria kuwa watu milioni 9.4 wanahitaji msaada.

“Wakati mzozo unavyoenea kaskazini mwa Ethiopia tunaona watu wengi zaidi wakiangukia katika hali mbaya,” Claire Neville, afisa wa WFP huko Addis alisema.

Alilaumu “mambo mengi” ambayo kwa sasa yanazuia ufikiaji wa misaada ya kibinadamu, ikiwa ni pamoja na mashambulizi ya waasi wa Tigray, ukosefu wa usalama, na ucheleweshaji unaoendelea kutoka kwa mamlaka ya Ethiopia.

Lakini WFP hivi karibuni imeweza kuwafikia maelfu ya watu katika miji miwili ya Amhara iliyotekwa na vikosi vya Tigray.

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha,

Wanawake hawa wako kwenye mkutano wa kuunga mkono vikosi vya serikali dhidi ya waasi wa Tigray

Vitani na ‘wasaliti’

Mjini Addis, chama tawala cha Prosperity kinaendelea kuandaa sherehe za hadhara za kuwashukuru wale wanaojitolea kupigana.

“Tuko vitani na wasaliti wa ndani, na wafadhili wao wa kigeni,” alisema Etisa Deme, mjumbe wa baraza la jiji.

“Niliitwa kwenda kupigania heshima ya nchi yangu, unaweza kulia familia yako ikiuawa, lakini ukiipoteza nchi yako unaenda wapi?

Ndiyo maana niko tayari kujitolea maisha yangu. Siogopi, “Sijapata mafunzo bado,” alisema kijana wa miaka ishirini na mbili, Babush Sitotaw.

Mwanamke mwenye mvi, Dinkinesh Nigatu, pia alijitokeza na kuwasilisha kwa umati. “Naipenda nchi yangu. Nilitaka kwenda mbele lakini mwanangu na mume wangu waliniambia nibaki nyumbani na watakwenda kupigana kwa niaba yangu,” alisema.

“Kwa hiyo nimepata mafunzo ya kujitolea na ninashika doria mitaani sasa hivi wanangu na mume wangu wanapigana kwenye mstari wa mbele.

Kila ninapoona watu mitaani, ninawaambia waende kupigana. Hatupaswi kusubiri mpaka ( adui) huja hapa kutuua sote,” aliiambia BBC.

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha,

Baadhi ya Waethiopia wanaandamana kupinga kile wanachokiita uingiliaji wa kigeni katika mzozo huo

Shutuma za ‘habari potofu za ukoloni mamboleo’

Serikali ya Ethiopia imelalamikia kampeni ya makusudi ya serikali za magharibi na mashirika ya vyombo vya habari kupotosha asili ya mzozo huo.

Waethiopia wengi wanaonekana kukubaliana, wakienda kwenye mitandao ya kijamii kukosoa majaribio ya “kikoloni” ya kudhoofisha taifa lao na kutilia chumvi mafanikio ya TPLF.

“Sisi tunashambuliwa kwa pande mbili. Kampeni ya upotoshaji wa ukoloni mamboleo na habari potofu za vyombo vya habari vya magharibi, ikiwa ni pamoja na BBC, na vita vya mauaji ya halaiki vilivyotangazwa na TPLF,” alisema mchambuzi wa kisiasa wa Ethiopia Achamyleh Ewunetu, ambaye alijieleza kuwa mkosoaji wa serikali ya Ethiopia lakini mtetezi wa uhuru wa nchi yake.

Serikali ya Ethiopia imekataa mara kwa mara maombi ya BBC ya mahojiano.

Lakini serikali ya Ethiopia imekosolewa pakubwa kwa kukandamiza vyombo vya habari vya ndani na nje ya nchi, kwa kuzuia ufikiaji na mawasiliano.

Waziri Mkuu Abiy, ambaye alisifiwa kabla ya mzozo kwa kuwaachilia wafungwa wa kisiasa na waandishi wa habari, hivi karibuni ameshutumiwa kwa kuweka tena mazingira ya vitisho kwa vyombo vya habari.

Wakati huo huo, BBC inasema inasalia kuwajibika kwa kutoa taarifa huru, sahihi na zisizo na upendeleo kutoka kanda na dunia nzima.

Zaidi kuhusu mzozo wa Tigray:

Source link

Author:

Leave a Reply

Your email address will not be published.